1. Mwanzo
  2. Jumbe
  3. 4 Agosti 2026

Majlisi ya Maombolezo ya Vikundi vya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu kwa Mnasaba wa Arbaini ya Imam Hussein, Karibu na Mahali pa Kuuawa Shahidi kwa Kiongozi Shahidi wa Iran

Hii ni tafsiri ya matini asilia ya Kiajemi. Matini asilia kwa Kiajemi

Katika majlisi hii, ambayo miaka iliyopita ilikuwa ikifanyika katika Husseiniya ya Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu) mbele ya Kiongozi shahidi wa Mapinduzi, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Tabatabaeinejad, katika hotuba yake, akiashiria vifungu vya Ziyara ya Arbaini ya Imam Hussein (amani iwe juu yake), alizungumzia athari za kuandamana na kuwa pamoja na walii wa Mwenyezi Mungu. Akitaja matunda ya kuandamana huko, alisema: Utakaso na kufanana na walii wa Mwenyezi Mungu, kupata maarifa na busara, kudhihirika kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu na moyo kujitoa katika nyoyo zilizo tayari, na saada ya dunia na akhera ni miongoni mwa matunda ya kuandamana na walii wa Mwenyezi Mungu; na sharti la kuandamana huko ni kujiepusha na kupita kiasi na uzembe, kwa namna ambayo mtu hapaswi kubaki nyuma ya walii wa Mwenyezi Mungu wala kutangulia mbele yake au kuingia katika misimamo mikali.

Katika majlisi hii pia, Bw. Meysam Motiei na Bw. Mahdi Rasouli walisoma nauha kwa kumlilia Bwana Aba Abdillah al-Hussein (amani iwe juu yake), Ahlul-Bayt watakatifu na masahaba wake waaminifu, na pia walisoma marthiya kwa ajili ya Kiongozi shahidi wa Mapinduzi.