Kuteuliwa kwa Dkt. Mohammad Bagher Zolghadr kuwa Mshauri wa Kisiasa wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi
Hii ni tafsiri ya matini asilia ya Kiajemi. Matini asilia kwa Kiajemi
بسم الله الرحمن الرحیم
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
Ndugu mheshimiwa, Dkt. Mohammad Bagher Zolghadr
Kwa kuzingatia uzoefu wako wenye thamani, kwa njia hii nakuteua wewe mheshimiwa kuwa Mshauri wangu wa Kisiasa. Natumaini kwamba katika kutekeleza jukumu hili na katika kuendeleza malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu, chini ya uangalizi wa Bwana wetu, Baqiyyatullah al-A'dham (Mwenyezi Mungu Mtukufu aharakishe faraja yake tukufu), utafanikiwa na kuungwa mkono.
Sayyid Mojtaba Khamenei