Kuteuliwa kwa Meja Jenerali Rubani Ali Abdollahi kuwa Mkuu wa Majeshi wa Vikosi vya Ulinzi
Hii ni tafsiri ya matini asilia ya Kiajemi. Matini asilia kwa Kiajemi
بسم الله الرحمن الرحیم
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
Meja Jenerali Rubani, mlinzi wa Mapinduzi, Ali Abdollahi
Kwa kuzingatia kuuawa shahidi kwa fahari na heshima kwa Luteni Jenerali shahidi Sayyid Abdolrahim Mousavi mikononi mwa adui wa Kizayuni na Kimarekani, na kwa kuzingatia huduma zako zinazostahili na uzoefu wako wenye thamani, nakuteua wewe mheshimiwa kuwa Mkuu wa Majeshi wa Vikosi vya Ulinzi.
Kutimizwa kwa kiwango cha juu kabisa kwa madai yafuatayo kunatarajiwa:
1. Kuinua uwezo na utayari wa kila upande na wa kisasa wa kiulinzi na kiusalama wa vikosi vya ulinzi na Basij ya wananchi
2. Kuandaa uwezo wa kujibu kwa wakati, kwa moyo wa kimapinduzi na kwa ufanisi kila kiwango na aina ya vitisho vya kawaida na vipya vya kijeshi, kiakili na mseto dhidi ya mfumo mtakatifu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
3. Kukamilisha mchakato wa kuunganisha Makao Makuu ya Vikosi vya Ulinzi na Kamandi Kuu ya Khatam al-Anbiya (rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na Aali zake) kwa msingi wa uamuzi wa Imam shahidi (radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu ziwe juu yake)
Inatumainiwa kwamba kwa inayaya za Mwenyezi Mungu, na chini ya kivuli cha dua zenye kheri na baraka za Bwana wetu (Mwenyezi Mungu Mtukufu aharakishe faraja yake tukufu), taufiki zaidi na aina mbalimbali za ushindi na nusura zitapatikana kwa vikosi vyote vya ulinzi vya mfumo wa Kiislamu.
Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei