Hii ni tafsiri ya matini asilia ya Kiajemi. Matini asilia kwa Kiajemi

بسم الله الرحمن الرحیم
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

Ndugu mtukufu, Mheshimiwa Dkt. Mohsen Rezaei

Kwa kuzingatia uzoefu wako wenye thamani, kwa barua hii nakuteua wewe, uliye miongoni mwa watangulizi wa kipindi cha fahari cha miaka minane ya Kujihami Kutakatifu, kuwa mwakilishi wangu katika Baraza Kuu la Usalama wa Taifa. Natumaini utapata mafanikio kamili katika kutekeleza jukumu hili muhimu.

Aidha, natoa shukrani kwa juhudi za usiku na mchana za ndugu mpendwa, Mheshimiwa Dkt. Mohammad Bagher Zolghadr.

Inshallah, chini ya umakini wa Bwana wetu, Hazrat Baqiyyatullah al-A'dham (Mwenyezi Mungu aharakishe faraja yake tukufu), daima uwe askari mwanajihadi kwa ajili ya taifa lenye fahari la Iran.

Sayyid Mojtaba Khamenei