Hii ni tafsiri ya matini asilia ya Kiajemi. Matini asilia kwa Kiajemi

بسم الله الرحمن الرحیم
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

Komodoo Ali Azmaei, wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi

Kwa kuzingatia kuuawa shahidi kwa fahari na heshima kwa Admirali Alireza Tangsiri, wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi, mikononi mwa adui wa Kizayuni-Kimarekani, na kwa kuzingatia kujitolea kwako, ustahiki wako na uzoefu wako wenye thamani, na kwa pendekezo la Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi, nakuteua kuwa Kamanda wa Kikosi cha Majini cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Kunatarajiwa kuimarisha mafunzo na ujuzi, zana na nyenzo za majini, umahiri wa kiintelijensia sambamba na kukuza uwezo na utayari wa kivita, kuinuka kiroho na kiufahamu, na kuzingatia mahitaji ya kimaisha kwa ajili ya kufikia kikosi cha majini chenye kiwango cha Mapinduzi ya Kiislamu, pamoja na ushirikiano wenye ufanisi na unaokamilishana na vipengele vingine vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi, Basij na Kikosi cha Majini cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na sekta nyingine husika za kijeshi na kiraia.

Inatarajiwa kwamba umakini na dua za Bwana wetu (Mwenyezi Mungu aharakishe faraja yake tukufu) zitakuletea wewe na wapiganaji wote wa kikosi hicho taufiki zinazoongezeka siku hadi siku.

Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei