Hii ni tafsiri ya matini asilia ya Kiajemi. Matini asilia kwa Kiajemi

بسم الله الرحمن الرحیم
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Hossein Taeb

Kwa kuzingatia kuuawa shahidi kwa fahari na heshima kwa Meja Jenerali Gholamreza Soleimani mikononi mwa adui wa Kizayuni na Kimarekani, na kwa kuzingatia uwajibikaji, ustahiki na uzoefu wako wenye thamani, na kwa pendekezo la Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi, nakuteua wewe mheshimiwa kuwa Mkuu wa Shirika la Basij ya Wanyonge (Basij-e Mostaz'afin) la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Kwa kuzingatia matakwa na mazingira mapya ya nchi, kutimizwa kwa madai yafuatayo, huku zikizingatiwa hatua za Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi, kunatarajiwa:

1. Kuimarisha na kupanua utamaduni wa Basij na muqawama kwa lengo la kutimiza kaulimbiu ya “Kila Mwirani, Mbasiji mmoja”, kwa kutumia uwezo wa wananchi wote walioamka na matabaka ya mamilioni ya walio tayari kujitoa mhanga, katika mwelekeo wa Iran yenye nguvu na umoja na kuyalinda Mapinduzi ya Kiislamu

2. Kuimarisha mtandao wa kiintelijensia wa wananchi, kuongeza ujuzi na mafunzo yanayohitajika sambamba na kuongeza mwamko na busara, na kutumia teknolojia mpya kwa ajili ya kukabiliana na vitisho vya adui kwa msingi wa wananchi

3. Ushirikiano wenye kujenga na wenye ufanisi na taasisi na mashirika mengine ya kiutawala, ya kiserikali na ya umma, na kupanua makundi ya jihadi, Basij ya matabaka na ya mitaa kwa lengo la kuendeleza huduma za kijamii zenye ufanisi, msikiti ukiwa ndio mhimili

4. Kueneza utamaduni wa Kibasiji kama kielelezo cha muqawama na uthabiti wa wananchi kote duniani dhidi ya ubeberu wa Kizayuni na Kimarekani

Inatumainiwa kwamba uangalizi na dua za Bwana wetu (Mwenyezi Mungu Mtukufu aharakishe faraja yake tukufu) zitakuwa sababu ya taufiki zinazoongezeka kila siku kwako na kwa Mabasiji wote wapendwa.

Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei