Pongezi kwa Ubingwa wa Dunia wa Timu ya Taifa ya Mieleka ya Kigiriki-Kirumi ya Chini ya Miaka 23
Hii ni tafsiri ya matini asilia ya Kiajemi. Matini asilia kwa Kiajemi
بسم الله الرحمن الرحیم
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
Ninawapongeza mabingwa hawa walioleta fahari, wakufunzi wenye bidii na wananchi wote wa Iran kwa ubingwa wa timu ya taifa ya Iran ya mieleka ya Kigiriki-Kirumi ya chini ya miaka 23 katika mashindano ya kimataifa ya vijana chipukizi wa dunia nchini Marekani.
Kung'ara kwa vijana wa nchi, kupepea kwa bendera ya Iran yenye kuamsha shauku na kurindima kwa wimbo wa taifa wa Jamhuri ya Kiislamu katika medani mbalimbali ni mng'ao wa matumaini ya taifa kwa vijana wake katika njia ya kufikia mustakabali angavu na adhimu.
Dua njema yangu inaambatana na safari ya vijana wote wa Iran tukufu.
Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei
25 Mehr 1405