Ujumbe kwa Mnasaba wa Kuzaliwa kwa Bibi Zainab na Siku ya Wauguzi
Hii ni tafsiri ya matini asilia ya Kiajemi. Matini asilia kwa Kiajemi
بسم الله الرحمن الرحیم
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
Tarehe tano Jamadil-Awwal kila mwaka inakumbusha kuzaliwa kwa baraka kwa bibi mtukufu ambaye alikulia chini ya kivuli cha mapenzi, malezi na kuambatana na Watu Watano Watoharifu (rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na juu yao), ambao wanahesabiwa kuwa bora zaidi ya viumbe vya Mwenyezi Mungu. Malezi na makuzi ya Zainab al-Kubra (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake) katika shule hii yenye nuru kwa kipindi cha zaidi ya miaka hamsini yalidhihirisha katika nyota hii inayong'aa ya zama zote madhihirisho mbalimbali ya vipengele vya utukufu na ubora, kiasi kwamba daima amekuwa chanzo cha kusifiwa, kupongezwa na kujivuniwa na mawalii wa Mwenyezi Mungu. Kilele cha mng'ao huu kilitokea katika tukio la kishujaa la Ashura: kwa upande mmoja, kutoa bila kikomo huruma, kuwatakia mema na kuwaliwaza kwa subira wale waliodhulumiwa katika uwanda wa Karbala; na kwa upande mwingine, kuwa miongoni mwa alama tukufu zaidi za uthabiti na ushujaa.
Historia ya harakati na Mapinduzi ya Kiislamu tangu mwanzo imejaa matukio ya kuwepo kwa wanawake na mabinti wa Iran kwa mwenendo wa Zainab. Jambo hili, katika kipindi cha mwamko usio na kifani wa taifa uliotokea katika Kujihami Kutakatifu kwa tatu, lilipata ubora na wingi wa kustaajabisha. Sasa wanawake wa Kizainabu wa Iran ya Kiislamu, kwa uwepo wao mkubwa katika nyanja mbalimbali, hasa katika viwanja vya mijini na vijijini, ni waanzilishi wa ubainishaji wa kivitendo na wa muqawama nyuma ya mistari ya vita vikali; kiasi kwamba madhalimu (twaghuti) wa zama hizi, ambao daima wanataka mateso, maumivu na ukandamizaji wa taifa hili, hawaoni ndani yao uwezo wa kukabiliana na jeshi hili kubwa.
Watu wa nchi ambayo inaipenda kwa dhati Itrah Toharifu (rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao wote), kwa kuzingatia upande wa upole, kuwahurumia wenye maumivu na kujitolea kwa ajili yao, kwa haki wameifanya siku ya kuzaliwa kwa Zainab al-Kubra kuwa siku ya kuenzi hadhi ya muuguzi. Kwa sababu sifa nyingi hizi za kimaadili na thamani za kibinadamu zinaonekana wazi katika tabaka la wauguzi wachapakazi na wenye thamani. Nafasi ya muuguzi, kama ilivyo kwa baadhi ya matabaka mengine kama madaktari, walimu na walezi, wanazuoni wa dini na waokoaji, ni nafasi ya kuhuisha na kuleta matumaini. Kwa sababu hiyo, muuguzi wakati mwingine hutazamwa kama malaika wa rehema, na hilo ni pale ambapo, mbele ya ukali na kukosa subira kwa watu wenye maumivu na wanaoteseka, huleta utulivu, matumaini, nafuu na tiba kwa wagonjwa, na matokeo yake kushuka kwa rehema ya Mwenyezi Mungu. Bila shaka nafasi ya wauguzi katika matibabu ya wagonjwa, tofauti na madaktari, inahitaji uwepo wa kudumu, wa ufuatiliaji na wa subira. Athari ya uwepo wa aina hii inavuka mambo ya kimwili, na itakuwa dawa ya maumivu ya kisaikolojia na kiroho, na kizuizi cha kukata tamaa kutawala katika matukio mengi. Ni kwa namna hii ambapo kile kilicho nje ya uwezo wa madaktari hukamilishwa kwa kutekeleza nafasi hii ya huruma.
Katika zama ambazo mtandao muovu wa uistikbari haujizuii na juhudi yoyote ya kuyaletea mataifa huru na yanayosimama imara, hasa taifa la Iran, aina zote za dhuluma na jinai, na miongoni mwa njia zake ni kuweka vikwazo vya aina mbalimbali vinavyohusiana na matibabu na dawa kwa lengo la kulilazimishia mateso taifa kubwa la Iran, kuwajali wauguzi, kuimarisha jamii ya wauguzi, kuhifadhi na kuinua elimu, ujuzi, uwezo, uchangamfu, hamasa na heshima ya wauguzi, hasa wale waliojitolea kufanya kazi katika taasisi zisizo za binafsi, kuna athari muhimu kwa afya na usalama wa kimwili na kiroho wa jamii. Kwa hiyo inatarajiwa kwamba viongozi wa sekta ya afya, kwa kuendeleza mienendo yao ya kujitolea, watayapa mambo haya muhimu kipaumbele.
Ninalipongeza taifa pendwa, wanawake wanaotambua wajibu wao na wenye azma kubwa wa nchi ya Kiislamu, na hasa dada na kaka wauguzi kwa minasaba hii miwili.
Mwishoni, namwomba Mwenyezi Mungu awarehemu mashahidi waliodhulumiwa na waliojitolea wa jamii ya wauguzi, hasa wauguzi waliouawa shahidi katika vita vya pili na vya tatu vilivyolazimishwa na katika fitina ya mwezi wa Dey 1404, na natumaini kwamba kwa dua ya Bwana wetu (Mwenyezi Mungu Mtukufu aharakishe faraja yake tukufu), Mwenyezi Mungu Mtukufu atalijaalia taifa la Iran izza na nguvu zaidi kuliko hapo awali na kila linalostahili kwa kufuata shule ya Zainab (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake).
Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei
24 Mehr 1405