Ujumbe wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu Wamtembelea Ayatullah Nouri Hamedani Hospitalini
Hii ni tafsiri ya matini asilia ya Kiajemi. Matini asilia kwa Kiajemi
Ujumbe kwa niaba ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, mchana wa leo, ulimtembelea Ayatullah Nouri Hamedani hospitalini.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Rahimian, Mohammadi Araghi, Mohammadian na Haj Ali Akbari, mchana wa leo walifika katika mojawapo ya hospitali za Tehran, na mbali na kufikisha salamu za Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Ayatullah Nouri Hamedani, mmoja wa Marajii wakuu wa Taqlid, walipata taarifa kuhusu maendeleo ya hivi karibuni ya matibabu yake.
Wawakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu pia walimtakia Ayatullah Nouri Hamedani apone haraka, na wakaeleza matumaini yao kwamba hawza za kielimu zitanufaika tena hivi karibuni na fadhila za kielimu za Marjaa huyu mtukufu.