Hii ni tafsiri ya matini asilia ya Kiajemi. Matini asilia kwa Kiajemi
بسم الله الرّحمن الرّحیم
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
Usalama ni miongoni mwa neema muhimu zaidi za Mwenyezi Mungu, na kudumishwa kwake katika maeneo mbalimbali ya Iran pendwa, kuanzia miji mikubwa hadi vitengo vidogo kabisa vya makazi vijijini na mitaani, kuanzia ulinzi mgumu wa mipaka katika hali ngumu za hewa na tabianchi mbalimbali za milimani hadi baharini, kuanzia nyanda na misitu hadi maeneo ya katikati kabisa ya nchi, kunatokana na ushujaa na ujasiri wa askari wanaojitolea na wachapakazi wa Polisi (FARAJA) kama mojawapo ya nguzo imara za usalama wa nchi.
Usalama huu huleta nyanja mbalimbali za kijamii, kimaadili na utulivu wa umma katika jamii, na huduma hiyo yenye thamani, mbali na kuwa jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, ina uungwaji mkono mkubwa wa kijamii. Nafasi kubwa ya FARAJA katika ngazi mbalimbali, kuanzia ngazi za uongozi na makao makuu hadi vituo vya polisi na vituo vya ulinzi, kwa ajili ya kudhamini usalama imezidi kujitokeza katika miaka ya hivi karibuni, na ishara za athari hii zilidhihirika zaidi katika vita vya pili na vya tatu vilivyolazimishwa. Kuzingatia na kung'ang'ania kwa adui mhalifu wa Kimarekani-Kizayuni kuzipiga ngazi mbalimbali za FARAJA, kuanzia ngazi za juu kabisa hadi vikosi vyake vya mstari wa mbele, pia kumeudhihirisha zaidi kuliko hapo awali umuhimu wa taasisi hii. Lakini juhudi hizi za kukata tamaa na mapigo maovu dhidi ya nguzo za utulivu na usalama wa jamii, ambayo hayana mfano wake katika historia, hayakuwafanya askari mashujaa wa FARAJA kurudi nyuma hata chembe katika jukumu lao, na hata katika mitaa na ndani ya magari, walitekeleza nafasi na majukumu yale yale waliyokuwa wakiyatekeleza katika maeneo na vituo vyao.
Kwa sababu hiyo, taifa la Iran lililodhulumiwa na lenye nguvu linathamini juhudi na jitihada zisizokoma za watumishi wa usalama wa nchi, na kwa upande mwingine askari wa FARAJA, ambao kama Jeshi la Taifa na Sepah wanatoka katika kina cha jamii, kwa mwenendo wao wa kujenga imani wanaweza kuongeza imani ya wananchi kwa taasisi hii yenye thamani. Huenda mara nyingi juhudi na kujitolea kwa walinzi wa usalama kukachukuliwa na baadhi ya watu kuwa ni jambo la kawaida, na ni hali hii ya kudhulumiwa na kutojulikana ndiyo inayoongeza malipo yao mbele ya Mwenyezi Mungu. Kuimarishwa kwa pande zote kwa vikosi vinavyolinda usalama katika nyanja mbalimbali za rasilimali watu, vifaa na programu, hasa kuboresha teknolojia, ikiwa ni pamoja na matumizi yenye malengo ya akili mnemba katika uchambuzi wa data, kuna nafasi muhimu katika ubora na urahisishaji wa utekelezaji wa majukumu ya FARAJA.
Kwa kumwomba Mwenyezi Mungu awainulie daraja na awaridhie mashahidi watukufu wa FARAJA, na kwa kuzishukuru familia zote na wafanyakazi, askari, na vikosi shupavu na mashujaa, hasa kamanda shujaa, asiyechoka na mwerevu wa FARAJA na jihadi zake; natumaini kwamba kwa dua ya Bwana wetu (Mwenyezi Mungu Mtukufu aharakishe faraja yake tukufu), watafanikiwa zaidi kuliko hapo awali katika kuinua usalama, nguvu na izza ya Iran ya Kiislamu.
Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei
16 Mehr 1405