Ujumbe wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu Wamtembelea Ayatullah Wahid Khorasani Hospitalini
Hii ni tafsiri ya matini asilia ya Kiajemi. Matini asilia kwa Kiajemi
Ujumbe kwa niaba ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, jioni ya leo, ulimtembelea Ayatullah Wahid Khorasani hospitalini.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Rahimian, Mohammadi Araghi na Haj Ali Akbari, jioni ya leo walifika katika mojawapo ya hospitali za Tehran, na mbali na kufikisha salamu na dua za Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, walipata taarifa kuhusu hali ya matibabu ya Ayatullah Wahid Khorasani, mmoja wa Marajii wakuu wa Taqlid.
Ayatullah Wahid Khorasani alipelekwa hospitalini kufuatia ugonjwa na amelazwa katika chumba cha uangalizi maalumu.