Agizo la Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Walioteuliwa na Kiongozi Shahidi Kuendelea na Kazi kwa Mujibu wa Hati na Maelekezo ya Awali
Hii ni tafsiri ya matini asilia ya Kiajemi. Matini asilia kwa Kiajemi
بسمهتعالی
Kwa jina Lake Aliye Juu.
Kufuatia maswali ya baadhi ya wakurugenzi na viongozi wa vyombo walioteuliwa moja kwa moja na Kiongozi shahidi (Mwenyezi Mungu aitakase roho yake safi), kwa njia hii natangaza kwamba kwa sasa hakuna yeyote kati yao anayehitaji kufanyiwa upya hati ya uteuzi, na ni lazima waendelee na kazi zao kwa msingi wa maelekezo na sera walizopokea wakati wa uhai wa mtukufu huyo.
Namwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awajaalie wote taufiki katika kutekeleza majukumu yao.
Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei