Ujumbe kwa Mnasaba wa Kusindikizwa na Kuzikwa kwa Bwana Shahidi wa Iran
Hii ni tafsiri ya matini asilia ya Kiajemi. Matini asilia kwa Kiajemi
بسم الله الرّحمن الرّحیم
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
السَّلامُ علیکَ یا ثاراللهِ وَ ابنَ ثاره وَ الوِترَ المَوتور. السَّلامُ علیکَ وَ علی جَدِّکَ وَ اَبیکَ وَ اُمِّکَ وَ اَخیکَ وَ المَعصومینَ مِن وُلدِک.
Amani iwe juu yako, ewe damu ya Mwenyezi Mungu na mwana wa damu Yake, na mpweke aliyedhulumiwa ambaye kisasi chake hakijalipwa. Amani iwe juu yako na juu ya babu yako, baba yako, mama yako, ndugu yako na Maasumina miongoni mwa wanao.
Amani iwe juu ya Imam ambaye mwito wa kuhuisha wa harakati yake uliupanua mwangwi mkubwa na wenye kurindima wa utume wa Mtume hadi kina cha mbali kabisa cha historia, na kutokana na athari yake yakazaliwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Mapinduzi ambayo kwa msingi wake yalikuwa ya Kihusseini, na yalijengwa na kukua kwa kaulimbiu na mwenendo wa Husein. Bwana shahidi wa Iran naye alikua kwa mwenendo huu huu. Alikuwa wa Kihusseini, alifikiri Kihusseini, alisonga mbele Kihusseini, alifanya jihadi na muqawama Kihusseini, aliishi Kihusseini, na Kihusseini alitoa damu yake katika njia ya shule ya Husein na akauawa shahidi. Miongoni mwa wafuasi wa Husein wapo wale ambao, damu yao inapomwagika ardhini kwa kudhulumiwa katika njia ya Husein na kwa ajili ya shule na mwenendo wa Husein (amani iwe juu yake), Umma wa Kiislamu huinuka, na wakati huo huunganika na Ashura na mahali hapo huunganika na Karbala. Sasa pia hamasa ile ile ya Kihusseini imelipa taifa letu mwamko na kuipa Shule ya Khomeini Mkuu na Khamenei shahidi mwonekano mpya. Hii ndiyo ile ghasia yenye kuhuisha ambayo mwangwi wa mwito wa kudhulumiwa kwa Husein (amani iwe juu yake) na mwito wake wa هَل مِن ناصرٍ یَنصُرُنیِ (Je, yupo msaidizi wa kunisaidia?) huianzisha nchini Iran na baada yake nchini Iraq na nchi nyingine, na kutikisa batili kwa tetemeko. Na inafaa kwa mnasaba huu nitoe shukrani za dhati kwa kuwepo kwa makumi ya mamilioni ya wananchi, kwa namna ya kustaajabisha, inayomvunja adui na ya kihistoria, katika miji na vijiji vya Iran na Iraq, hasa Tehran, Qom, Najaf, Karbala na Mashhad.
Taifa letu linadai kisasi cha damu ya Husein. Taifa hili kubwa kwa miaka mingi limetoa mhanga watoto wake katika njia ya Husein na katika vita dhidi ya maadui wa Husein na mwenendo wa Kihusseini. Na sasa pia linadai kisasi cha damu yake na ya wafuasi wa Husein wa zama hizi.
Sasa namwambia kiongozi wetu shahidi: Ewe uliyeuawa kwa kudhulumiwa! Ewe uliyedhulumiwa mwenye heshima! Ewe mja mwema wa Mwenyezi Mungu! Sasa ambapo kwa macho yanayotiririka machozi na nyoyo zilizovunjika tunauaga mwili wako, tunafunga nawe agano kwamba tutailinda shule yako, na tutaipita kwa msimamo ile njia iliyonyooka uliyoichora, na katika njia hii hatutaogopa mashaka, na kama wewe tutazitegemea bishara na ahadi za Mwenyezi Mungu. Tunafunga agano kwamba tutalipiza kisasi cha damu yako safi na ya mashahidi wote wa vita hivi viwili kutoka kwa wauaji wahalifu na wasio na heshima. Kisasi hiki ni matakwa ya taifa letu na ni lazima kitekelezwe kwa uhakika. Wahalifu hawa, ambao orodha yao kuanzia wa juu hadi wa chini ipo, watakwenda kaburini na matamanio ya kufa kifo cha utulivu kitandani. Wanapaswa kujua kwamba jambo hili halitegemei kuwepo kwangu binafsi wala kwa viongozi wengine. Tuwepo au tusiwepo, jambo hili litatimia, na punde watu huru kote duniani, kila mmoja atatekeleza sehemu ya jukumu hili la kiungu.
Ewe baba shahidi wa umma, hongera kwa kunywa asali ya kuuawa shahidi ambayo uliitamani umri wako wote. Hongera kwa kuvaa vazi la kuuawa shahidi kwa mwili wenye alama kutoka kwa mama yako Zahra mtoharifu, babu yako Abu Abdillah al-Husein na Abul-Fadhl al-Abbas (rehema na amani ziwe juu yao). Na ninyi, enyi wenzake waliodhulumiwa mliovamiwa ghafla na adui na mkauawa shahidi, heri yenu kwamba sasa ni wageni wa Bwana yule ambaye huenda mara nyingi mlionja upole na fadhila zake. Bwana yule ambaye ni mlango wa rehema ya Mwenyezi Mungu kwa wote, na hasa kwa watu wa ardhi hii, sasa ndiye mwenyeji wenu, na ujirani wake salama umekuwa nyumba yenu.
Na wewe, ewe Bwana mwenye daraja ya juu! Ewe mtukufu! Ewe Imam mwenye huruma! Ewe Abal-Hasan ar-Ridha al-Murtadha, rehema bora za Mwenyezi Mungu ziwe juu yako; sasa mwili uliokatwa vipande vipande wa mmoja wa watumishi wako na wa kizazi kitoharifu, baada ya miaka mingi ya bidii, juhudi na jihadi isiyokoma, pamoja na miili ya mashahidi kutoka katika familia yake, ambao kila mmoja anamkumbusha mmoja wa mashahidi wa uwanda wa Karbala, wanapumzika katika udongo huu safi hadi siku ile ambapo, kwa amri ya Mwenyezi Mungu, jua linaloangaza ulimwengu, Baqiyyatullah (Mwenyezi Mungu Mtukufu aharakishe faraja yake tukufu), litatoka nyuma ya mawingu ya ghaiba na kuwaangazia watu wa sayari hii nuru ya rehema ya Mwenyezi Mungu. Siku hiyo, ambayo tunatumaini itafika hivi karibuni sana, nyota kutoka miongoni mwa wakweli, mashahidi na mawalii watamwandama mtukufu huyo, na tunatumaini kwamba Bwana wetu shahidi atakuwa mmoja wao, na kwa mara nyingine ataonyesha matukio ya kung'aa na safi ya jihadi na utekelezaji wa agano la Alast, na huenda wenzake hawa watamwandama tena siku hiyo.
Ewe Bwana mwenye huruma! Tunamkabidhi kwako, kwa fadhila na inayaya yako, Bwana wetu aliyetumia kila kitu chake katika njia yako, pamoja na wenzake mashahidi, ili kama walivyonufaika na fadhila yako katika maisha yao ya dunia, kuanzia sasa pia wanufaike vivyo hivyo, bali kwa kiwango cha juu zaidi na zaidi.
Mwisho, kwa mara nyingine tunatoa rambirambi kwa Bwana wetu Baqiyyatullah (Mwenyezi Mungu Mtukufu aharakishe faraja yake tukufu), na tunamwomba mtukufu huyo mwenye huruma aelekeze dua zake safi kwa Bwana shahidi wa Iran, wenzake mashahidi na mashahidi wote, na amwombe Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na Mtukufu, daraja za juu kwa mashahidi wote, subira na ujira kwa familia zao, na ushindi na nusura ya uhakika na ya karibu kwa taifa linalodhulumiwa la Iran, In sha Allah.
Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei
18 Tir 1405