Hii ni tafsiri ya matini asilia ya Kiajemi. Matini asilia kwa Kiajemi

بسم الله الرّحمن الرّحیم
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

لبَّیک اللّهمّ لبَّیک، لبَّیک لا شریک لک لبَّیک، إنّ الحمد و النّعمة لک و المُلک...

Ewe Mwenyezi Mungu! Naitikia wito Wako, Wewe huna mshirika yeyote, na sifa zote, neema zote na ufalme wote na nguvu zote zinatoka Kwako na ni Zako...

Msimu wa Hija wa mwaka huu nao umewadia, na mahujaji wa Umma wa Kiislamu wamevaa ihramu ya utumwa kwa Mwenyezi Mungu na kusoma talbiya ili wahame kutoka katika maisha ya kimaada na ya kawaida kwenda kwenye maisha ya kiungu na yenye saada; maisha ya tawhidi yanayozunguka mhimili wa kumwabudu Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na Mtukufu, na kuwakataa, kuwapinga na kujitenga na wanaofanywa washirika wa Mwenyezi Mungu. Lakini fursa ya hijra hii si ya mahujaji na wageni wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu wa mwaka huu peke yao, bali inawajumuisha ndugu wote wa kiume na wa kike wa Kiislamu nchini Iran na kote duniani, kuanzia wale waliokwisha hiji katika miaka iliyopita ya umri wao hadi wale ambao bado hawajapata taufiki ya kutekeleza ibada za Hija.

Sharti la hijra hii ni kuvaa ihramu ya kudumu kuzunguka dhikri ya Mwenyezi Mungu; ni tawafu ya kudumu kuzunguka mhimili wa haki; ni sa'yi ya kudumu kati ya vilele vizito vya majukumu ya kiungu; ni kumpiga mawe daima shetani mwovu pamoja na madhihirisho yake ya kupotosha na wafuasi wake wote; ni kisimamo (wuquf) kilichochanganyika na tafakuri na unyenyekevu; ni kumlisha fakiri asiyejiweza na msafiri; ni kuchinja matamanio na mielekeo inayopotosha na kuondoa uchafu wa ndani; na katika hali zote, ni kuwa tayari kutumikia na kupeperusha bendera ya kuitetea haki.

Na hivi ndivyo taifa la Iran, katika miqati ya Mapinduzi ya Kiislamu, lilivyoanza safari ya hijra hii, likaitikia wito wa Kiibrahimu wa Khomeini Mkuu, likavua vazi la kukubali kutawaliwa, likavaa ihramu ya saada ya dunia na akhera, na huku likisema labbayk na likienda kwa haraka, lilijitahidi kutufu kuzunguka mhimili wa maarifa ya Uislamu safi wa Muhammad (rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na Aali zake) na kujikurubisha kwenye nuru inayoangaza ulimwengu ya uadilifu wa kimataifa na wilaya kuu. الله اکبر، الله اکبر، لا اله الا الله والله اکبر، الله اکبر ولله الحمد، الله اکبر علی ما هدانا (Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mkubwa; Mwenyezi Mungu ni Mkubwa na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu; Mwenyezi Mungu ni Mkubwa kwa kutuongoa).

Ndiyo, الله اکبر (Mwenyezi Mungu ni Mkubwa)... Na ni kwa silaha hii hii ya Allahu Akbar ambapo taifa la Kiislamu la Iran lilisimama miaka arobaini na saba iliyopita, likauangusha utawala wa kitaghuti, wa kidikteta na tegemezi wa Pahlavi, likakata mikono na miguu ya Marekani yenye tamaa na kiburi kutoka nchini, na likakata kabisa ushawishi wa Uzayuni.

Ni kwa silaha hii hii ya Allahu Akbar ambapo, baada ya uvamizi wa utawala wa Kibaath wa Saddam katika ardhi ya Iran, wapiganaji shupavu wa jihadi na vijana waliojitolea waliandika ushujaa wa miaka minane ya Ulinzi Mtakatifu, na licha ya kuungwa mkono kwa utawala wa Kibaath na madola yote ya Mashariki na Magharibi, walimrudisha mahali pake; na waliendeleza msimamo huu kwa uthabiti na uimara kwa miaka mingi baadaye mbele ya mizingiro ya kiuchumi, mapinduzi ya kijeshi, vikwazo vya kidhalimu na mashambulizi yasiyohesabika ya kisiasa, kipropaganda na kiuchumi ya maadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

والله اکبر (Na Mwenyezi Mungu ni Mkubwa)... Ni silaha hii hii ya Allahu Akbar iliyoimarisha mafungamano ya Umma wa Kiislamu na vijana wapiganaji wa jihadi wa Mhimili wa Muqawama, kuanzia Iran hadi Lebanon, Palestina, Iraq na Syria, kuanzia Afrika na Yemen hadi Afghanistan na Pakistan na mataifa yote huru ya dunia, ili kamba hii madhubuti isimame kutetea uhai wa Umma wa Kiislamu dhidi ya wavamizi wanyang'anyi wa Kizayuni, ikunje daftari la Daesh (ISIS), ianzishe Tufani ya Al-Aqsa na kuufanya utawala wa Kizayuni uliotetereka kuhema kwa shida.

الله اکبر (Mwenyezi Mungu ni Mkubwa); ndiyo, Mwenyezi Mungu, Aliyebarikiwa na Mtukufu, ni Mkubwa kuliko kuweza kusifiwa... Ni silaha hii ya Allahu Akbar ambayo kwa kuitegemea, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilifanikiwa katika vita vya pili vilivyolazimishwa mwezi Khordad 1404 kuufanya utawala wa Kizayuni usiwe na la kufanya chini ya mapigo yake makali, kuipiga Marekani mvamizi kofi kali, na kumfanya adui ashindwe katika lengo lake la kuifanya Iran isalimu amri.

Na silaha ya Allahu Akbar iliwapa wananchi wa Iran nguvu na uwezo kiasi kwamba, baada ya tukio linalounguza moyo la kuuawa shahidi kwa Kiongozi Mtukufu, mwana mwema wa Mtume Mtukufu (rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na Aali zake), Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Hosseini Khamenei (Mwenyezi Mungu ainue daraja yake tukufu), mikononi mwa waovu wa dunia ya leo, lilipata mwamko wa kiungu, na kwa uwepo wake wa kila upande katika kila uwanja uliohitajika, liliyashangaza macho ya dunia kwa mafanikio yake ya fahari.

الله اکبر (Mwenyezi Mungu ni Mkubwa); hakika Mwenyezi Mungu, Aliyebarikiwa na Mtukufu, ni Mkubwa kuliko kuweza kusifiwa... Ni kwa silaha hii hii ya Allahu Akbar ambapo wapiganaji shupavu na vikosi vya ulinzi vilivyo tayari kujitoa mhanga katika Iran ya Kiislamu, pamoja na wapiganaji wa jihadi wa Mhimili wa Muqawama, hasa Lebanon pendwa, walipata ushindi mkubwa dhidi ya majeshi mawili ya kigaidi ya Marekani na Kizayuni yaliyojizatiti kwa silaha hadi meno katika vita vya tatu vilivyolazimishwa; kwa kumtegemea Mola, na kwa makombora na ndege zao zisizo na rubani ardhini, angani na baharini, walimpiga mawe Shetani Mkubwa, yaani Marekani, na mnyama wake aliyefugwa, utawala wa Kizayuni, na wakaiona kwa macho yao ahadi ya kweli ya Mwenyezi Mungu ya kuwanusuru wanaofanya jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Na tena الله اکبر (Mwenyezi Mungu ni Mkubwa); bila shaka Mwenyezi Mungu, Aliyebarikiwa na Mtukufu, ni Mkubwa kuliko kuweza kusifiwa, na majeshi Yake yanashinda kila nguvu... Na ni kwa silaha hii hii ya Allahu Akbar ambapo, kufuatia mwamko wa taifa la Iran na Mhimili wa Muqawama, mwamko wa Umma wa Kiislamu utatimia, na kujitenga na washirikina kutavuka kutoka katika kupiga mawe Jamarat za Hija hadi katika nyanja za maisha ya kibinafsi, kijamii na kisiasa ya Waislamu katika pembe za mbali kabisa za dunia.

Umma wa Kiislamu na mataifa ya eneo hili yana uwezo na maslahi mengi ya pamoja ambayo yataunda mpangilio mpya na jiometri ya mustakabali wa eneo na dunia. Mimi, kwa ukweli na ikhlasi, nazilingania nchi na serikali zote za Kiislamu kwenye urafiki na kusaidiana katika kheri na wema, ili kwa kushirikiana tupige hatua katika njia ya maendeleo ya Umma wa Kiislamu na kutatua masuala ya ulimwengu wa Kiislamu.

Kilicho hakika katika uwanja huu ni kwamba mshale wa saa haurudi nyuma, na mataifa na ardhi za eneo hili hayatakuwa tena ngao ya kambi za kijeshi za Marekani. Marekani, mbali na kwamba haitakuwa tena na mahali salama kwa ajili ya uovu na kuweka kambi za kijeshi katika eneo hili, siku baada ya siku inazidi kujitenga na hali yake ya awali. Utawala wa Kizayuni uliotetereka na saratani ya Israel nao umekaribia hatua za mwisho za umri wake wa nuksi, na kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu, na kwa mujibu wa kauli thabiti na ya kuona mbali ya Kiongozi Mtukufu shahidi (Mwenyezi Mungu aitakase roho yake safi) ya miaka kumi iliyopita (1), hautaiona miaka ishirini na mitano baada ya tarehe ile, In sha Allah.

Kwa sababu hiyo, mwaka huu suala la kujitenga na washirikina lina umuhimu maradufu, na kina na upana wa kujitenga na Marekani na utawala wa Kizayuni unavuka mipaka ya ibada ya kujitenga katika msimu na miqati ya Hija; na katika sehemu mbalimbali za Iran na dunia, na baada ya siku hizi zenye baraka, “Mauti kwa Marekani” na “Mauti kwa Israel” itakuwa kaulimbiu iliyoenea ya Umma wa Kiislamu na wanaodhulumiwa duniani, hasa vijana.

Mustakabali ni wa Umma wa Kiislamu na ustaarabu mpya wa Kiislamu, na kila mmoja wetu anaweza, kwa kadiri ya himma, uwezo na jukumu lake, kutekeleza nafasi katika kufikia mustakabali huu na kuukaribia.

Wageni na mahujaji wa Kiirani katika Hija ya mwaka huu wana nafasi yenye athari na muhimu katika kuwasimulia ndugu zao wengine wa kiume na wa kike wa Kiislamu habari ya ushindi wa vita vya tatu vilivyolazimishwa, na kuwapa matumaini ya mustakabali mwema.

Nawaomba mahujaji wote wapendwa wajishughulishe na dua ya kuharakishwa kwa faraja ya Mwokozi wa wanadamu (Mwenyezi Mungu Mtukufu aharakishe faraja yake), na waombe dua kwa ajili ya umoja wa Umma wa Kiislamu, ukombozi wa Palestina na Msikiti wa Al-Aqsa, kuondolewa kwa matatizo makubwa ya Waislamu na kufikia ushindi wa mwisho dhidi ya ubeberu wa kimataifa, na wanijumuishe nami katika dua zao njema.

Ewe Mola! Mrehemu Muhammad na Aali wa Muhammad, na uwafikishie mahujaji na Umma wote wa Kiislamu jicho la upole na huruma Yako, uwajaalie taufiki ya Hija iliyokubaliwa, uziangaze nyoyo zao kwa nuru za maarifa na busara, na uifanye azma na irada yao kuwa thabiti zaidi katika kusonga mbele katika njia ya kurekebisha hali ya umma na ushindi wa mwisho dhidi ya maadui wa Uislamu.

Ewe Mola! Teremsha fadhila na rehema Yako pana juu ya roho takatifu za mashahidi wa njia ya Mwenyezi Mungu, hasa mashahidi wa Mhimili wa Muqawama, na wa kwanza wao Kiongozi Mtukufu shahidi (Mwenyezi Mungu ainue daraja yake tukufu); na kutokana na Hija ya mahujaji, ibada ya wanaoabudu na juhudi za wanaojitahidi waliokuwa chini ya uongozi na mwongozo wa Kiongozi wa umma, ifikishie roho yake ya kimalakuti sehemu kubwa; na lisaidie taifa la Iran na Umma wa Kiislamu katika kuendeleza njia na lengo lake.

Ewe Mola! Teremsha rehema na maamkizi Yako bora kabisa juu ya Bwana na Mola wetu, Imam Mahdi anayesubiriwa (rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na juu ya mababu zake watoharifu), na utujumuishe sisi sote na Umma wa Kiislamu katika dua zake safi na zenye kujibiwa, na uiangaze na kuipamba dunia kwa ujio wake wenye baraka kama ulivyoahidi, na nyoyo zetu zimejaa yakini juu ya ahadi hiyo isiyoepukika. «وَعَدَ الله الَّذینَ آمنوا مِنکُم وَ عَمِلوا الصّالِحاتِ لَیَستَخلِفَنَّهُم فی‌الارضِ کَما استَخلَفَ الَّذینَ مِن قَبلِهِم وَ لَیُمَکِّنَنَّ لَهُم دینَهُمُ اَلَّذِی ارتَضی لَهُم وَ لَیُبَدِّلَنَّهُم مِن بَعدِ خَوفِهِم اَمنا»
Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na wakatenda mema kwamba hakika atawafanya washike utawala katika ardhi kama alivyowafanya walioshika utawala wale waliokuwa kabla yao, na hakika atawaimarishia dini yao aliyowaridhia, na hakika atawabadilishia amani baada ya hofu yao. (Qur'ani, An-Nur 24:55)

والسّلام علی جَمیعِ اِخواننا المسلمین و رحمةالله و برکاته
Amani iwe juu ya ndugu zetu wote Waislamu, na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka Zake.

Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei
5 Khordad 1405
9 Dhul-Hijjah 1447

(1) Hotuba katika mkutano na matabaka mbalimbali ya wananchi, 1394/06/18