Jibu kwa Barua za Kundi la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu
Hii ni tafsiri ya matini asilia ya Kiajemi. Matini asilia kwa Kiajemi
باسمهتعالی
Kwa Jina Lake Aliyetukuka
Salamu kwa wanangu wapendwa;
Nimezisoma barua zenu zilizojaa mapenzi. Ninawashukuru kwa wema wenu mwingi, ninyi wanafunzi wa vyuo vikuu, vijana wenye ari kubwa, na kwa ajili yenu nyote mlioniwekea deni la shukrani, nitawaombea dua maalumu.
Katika barua zenu, na za vijana na wanafunzi wengi wa vyuo vikuu wanaonitendea mimi mnyonge wema na mapenzi yao, kunang'aa azma, irada na hisia ya uwajibikaji katika kujenga mustakabali. Agano hili madhubuti ni amana yenye thamani kubwa, yenye mizizi katika shule ya Uislamu safi wa Muhammad (rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na Aali zake) na urithi wa Khomeini Mkuu na Khamenei shahidi (Mwenyezi Mungu ainue daraja zao tukufu), nalo ndilo kamba inayotuunganisha sisi kwa sisi katika «kuwa na ahadi moja».
Kwa lengo hilo, jizatitini kadiri muwezavyo kwa silaha ya elimu na imani, utakaso wa nafsi, ukaribu na Mwenyezi Mungu na kuyajua kwa kina maarifa ya Qur'ani na Ahlul-Bayt (amani iwe juu yao), na kwa kazi na ubunifu maradufu ongezeni nguvu na uwezo wa Iran pendwa, ili kwa dua ya Bwana wetu mwenye huruma (Mwenyezi Mungu Mtukufu aharakishe faraja yake tukufu), safari ya majeshi yaliyofungamana katika ahadi moja kuelekea vilele vya maendeleo na ustaarabu wa Kiislamu-Kiirani ifanikiwe kwa ubora zaidi na kwa haraka zaidi, Inshallah.
Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei
6 Aban 1405